Skip to main content

Ban aipongeza Timor-Leste kwa kuendesha uchaguzi kwa amani

Ban aipongeza Timor-Leste kwa kuendesha uchaguzi kwa amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Timor-Leste kwa kuendesha uchaguzi katika mazingira ya amani hatua ambayo ameieleza kuwa ni kukaribisha machipuo mapya ya demokrasia.

Wananchi hao mwishoni mwa wiki walimiminika kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi wa rais, uchaguzi ambao unatoa mustakabala mpya wa taifa hilo.

 Ban amesema kuwa kwa kufuatilia hali ya mambo, uchaguzi huo ulifanyika katika mazingira ya utulivu na kwa kufuata taratibu zote za haki na hivyo ameahidi kuendelea kuiunga mkono nchi hiyo.

Taifa hilo la Timor-Leste baadaye mwaka huu linatazamia kuadhimisha mwaka wa 10 wa uhuru wake.