Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna kufikia malengo ya kimataifa bila uwajibikaji Rio+20:UM

Hakuna kufikia malengo ya kimataifa bila uwajibikaji Rio+20:UM

Kundi la wataalamu huru 22 wa haki za binadamu limeandika barua ya wazi likizitaka serikali kujumuisha mila, desturi na viwango vya kimataifa vilivyokubalika vya haki za binadamu pamoja na uwajibikaji wa hali ya juu katika malengo ya mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20 katikia majadiliano yake ya kwanza yalioanza Jumatatu mjini New York.

Wataalamu hao wameonya kwamba malengo ya kimataifa yanawekwa kirahisi lakini machache yanafikiwa, hivyo wametaka mkutano kuongeza msukumo wa nini cha kufikiwa.

Wameongeza kuwa hatari kubwa ni kwamba yatakayoafikiwa Rio yatasalia kuwa ahadi hewa bila ufatiliaji na uwajibikaji.

Wamesisitiza hayo zikiwa zimesalia chini ya siku 100 kabla ya mkutano wa Rio+20 kuanza.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)