Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM kuhusu masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake kuitembelea Papua New Guinea

Mjumbe wa UM kuhusu masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake kuitembelea Papua New Guinea

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya dhuluma dhidi ya wanawake, kinachosabisha dhuluma hizo na athari zake Rashida Manjoo anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Papua New Guinea kati ya tarehe 18 na 26 mwezi huu.

Manjoo amesema kuwa ataangazia dhuluma dhidi ya wanawake kwa upana wakati wa ziara yake, kinachosababisha dhuluma hizo na athari zake kwa wanawake, dhuluma ambazo zinachangiwa na nchi.

Mjumbe huyo pia atakutana na idara za  serikali na waakilishi wa mashirika ya umma kwenye maeneo ya Port Moresby, Goroka, Kundiawa, Minj na Buka ambapo pia atakutana na waathiriwa wa dhuluma za kijinsia.

Kisha baadaye atawasilisha ripoti ya  matokeo ya ziara yake na mapendekezo  kwenye kikao kinachokuja cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.