Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yakaribisha hatua ya Brazil ya kumfungulia mashtaka mwanajeshi wa zamani

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yakaribisha hatua ya Brazil ya kumfungulia mashtaka mwanajeshi wa zamani

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha uamuzi wa Brazil wa kumfungulia mashtaka mwanajeshi mmoja wa zamani kutokana na madai ya kutoweka kwa raia wakati wa utawala wa kijeshi nchini humo.

Hii ndiyo mara ya kwanza Brazil inawachukulia hatua wale wanaoaminika kutenda uhalifu na ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wa kijeshi uliodumu kwa muda wa miaka 21. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)