Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka uchaguzi wa amani na huru Guinea-Bissau

Ban ataka uchaguzi wa amani na huru Guinea-Bissau

Wakati wananchi wa Guinea Bissau wakielekea kwenye uchaguzi mkuu hapo siku ya jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kuwepo kwa hali ya amani na sura ya uwazi.

Jumla ya wagombea 9 akiwemo pia waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kumba Yala wanachuana kwenye kinyang’anyiro hicho.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha rais Malam Bacai Sanhá aliyeaga dunia miezi miwili iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika taarifa yake juu ya uchaguzi huo, Ban amezitaka pande zote zinazohusika kwenye uchaguzi huo, kuhakikisha unafanyika katika mazingira ya amani na uwazi.