Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD yaishauri serikali ya Haiti kuanzisha sera mpya za uwekezaji

UNCTAD yaishauri serikali ya Haiti kuanzisha sera mpya za uwekezaji

Wataalamu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa UNCTAD wamemshauri rais wa Haiti pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kuhusiana na uanzishwaji wa sera mpya ya uwekezaji nchini humo.

Ama wataalamu hao wametaka pia nchi hiyo kuifanyia mapitio sera yake ya uwekezaji iliyoko sasa.

Hatua hiyo inafuata baada ya wataalamu hao waliobobea kwenye uchumi wa kimataifa, kuwa na mkutano wa pamoja na maafisa wa serikali ya Haiti.

Serikali ya Haiti iliendesha kongamano la uwekezaji, kuanzia March 12 hadi 14 na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.

 Serikali hiyo ya Haiti imewaomba wataalamu hao kutoa msaada zaidi hasa katika maeneo ya kiufundi ili kusukuma mbele hali ya uchumi wa taifa hilo.