Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatimaye mahakama ya ICC yatoa hukumu yake ya kwanza

Hatimaye mahakama ya ICC yatoa hukumu yake ya kwanza

Jumatano wiki kwa mara ya kwanza mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC iliyoko The Hague Uholanzi imetoa hukumu yake ya kwanza kabisa tangu kuanzishwa na kuanza kushughulikia kesi za uhalifu wa vita.

Mahakama hiyo imemkuta na hatia mbabe wa zamani wa kivita kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga. Lubanga alishitakiwa kwa uhalifu wa vita na hasa kuwafunza na kuwaingiza watoto jeshini huko Ituri Congo kati ya mwaka 2002 na 2003. Baada ya hatia hiyo sasa huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha jela. Je watu wanasema aje kuhusu hukumu hiyo? Ungana na Flora Nducha katika makala hii.