Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni mwaka mmoja tangu wimbi la mabadiliko ya kihistoria nchini Syria:Ban

Ni mwaka mmoja tangu wimbi la mabadiliko ya kihistoria nchini Syria:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema leo ni mwaka moja tangu wimbi la mabadiliko ya Kihistoria kuikumba nchi ya Syria, raia waliposimama katika mitaa ya Damascus na kukata rufaa kwa ajili ya haki zao na uhuru kwa wote.

Baada ya siku chache maandamano ya amani yalianza mjini Deraa na kusambaa hadi maeneo mengine nchini kote. Serikali ya Syria ilianza ukandamizaji wa kikatili na ambao umeendelea bila kupungua. Matokeo haya ni ya kusikitisha kwa ulimwengu. Zaidi ya watu 8000 wameuawa kutokana na uamuzi wa serikali kuchagua ukandamizaji wa kutumia nguvu badala ya mazungumzo ya amani ya kisiasa ambayo yangeleta mabadiliko ya ukweli.

Ban amesema ni muhimu kusitisha vurugu, kuacha kutumia majeshi dhidi ya raia na kuzuia kuendeleza vita katika Syria. Hali ya Syria ni ya kusikitisha.

Ameongeza kuwa amesimama kwa mshikamano na watu wa Syria katika matarajio yao ya uhuru, utu na haki. Ametoa wito wa kusitisha machafuko, ili kutafuta suluhu ya mgogoro huu kwa njia ya amani. Ametoa wito kwa serikali ya Syria na upinzani kushirikiana pamoja na mjumbe maalum na kwa wito wa jumuiya ya kimataifa kutoa ushirikiano wa dhamira na umoja wa kuacha umwagaji damu na kupata suluhu ya kisiasa ambayo itaitikia matakwa ya watu wa Syria na kuhakikisha wanapata heshima kwa haki zao za msingi.