Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku

Katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku

Takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wamekufa kutokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku kote duniani, na hiyo ni sawa na kifo cha mtu mmoja kila baada ya sekunde sita.

Kwa mujibu wa ripoti  ya WHO maeneo ambayo yana kiwango kikubwa cha vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ni Marekani na bara Ulaya ambako tumbaku imekuwa ikitumika kwa muda mrefu zaidi.

Pia ripoti hiyo imebainisha kwamba tumbaku ndio mihadarati pekee iliyohalalishwa ambayo inawaua watu wengi wanaoitumia kama ilivyokusudiwa na wazalishaji.

Mwandishi wetu kutoka Burundi amepata maoni kuhusu matumizi ya tumbaku. Wasikilize....

 (SAUTI MAONI BURUNDI)