Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM apongeza viongozi wapya Ivory Coast

Mwakilishi wa UM apongeza viongozi wapya Ivory Coast

Mkuu wa Umoja wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast Bert Koenders amempongeza waziri mkuu mpya na Rais wa bunge wa nchi hiyo waliochaguliwa hivi karibuni na kuwahakikishia kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa UNOCI utaendelea kuwasaidia.

Jeannot Ahoussou Kouadio ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo huku bunge la taifa likimchagua Guillaume Soro kuwa Rais mpya wa bunge.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)