Mahiga alaani shambulio la kujitoa muhanga Mogadishu

Mahiga alaani shambulio la kujitoa muhanga Mogadishu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amelaani vikali shambulio la kujitoa muhanga katika lango la Villa Somalia upande wa serikali ya mpito mjini Moghadishu Jumatano jioni.

Mahiga ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa kuwatakia nafuu ya haraka.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limekiri kuhusika na amelitaka kusitisha mara moja mashambulizi ambayo yanaendelea kuathiri maelfu ya raia wasio na hatia na kukatili maisha ya watu.

Mahiga amewataka wananchi kuwa makini na kuwaahidi kwamba vitendo kama hivyo vya kigaidi havitovuruga mchakato wa amani.

Ameitaka serikali ya mpito kutoa msaada kwa waathirika mashambulio ya kigaidi na kuimarisha jeshi la serikali.