Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi watatu wa kulinda amani wa UM wamerejeshwa nyumbani kutoka Haiti

Wanajeshi watatu wa kulinda amani wa UM wamerejeshwa nyumbani kutoka Haiti

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakihudumu nchini Haiti wamerejeshwa nyumbani kufuatia kesi iliyokuwa ikiwakabili wa inayohusiana na kulawitiwa kwa kijana mmoja wa kiume mwenye umri wa 14.

Walinda amani hao kutoka Pakistan wanaohudumu kwenye kikosi cha polisi kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha MINUSTAH walikuwa wakihudumu kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi wa Gonaives. Ripoti kutoka utawala wa Pakistan zinasema kwamba huenda wanajeshi hao wakafukuzwa kazi na kufungwa mara watakaporejea Pakistan.