Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu watawanywa na mapigano Gedo, Somalia

Maelfu watawanywa na mapigano Gedo, Somalia

 

Taarifa kutoka Somalia zinasema maelfu ya watu wametawanya na mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa Al-Shabab na majeshi ya Somalia yanayosaidiwa na Ethiopia na wanajeshi wa Kenya katika jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia la Gedo.

Kwa mujibu wa gavana wa Gedo Mohamed Adi Kalili katika wiki chache zilizopita watu 5000 zaidi wametawanywa na machafuko hayo huku mamia ya familia zilikuwa tayari zimefunga virago kukimbia vita.

Ameongeza kuwa mapigano hayo yamekata kabisa biashara baina ya jimbo hilo na Moghadishu na mji wa Baidoa, na huduma za jamii zikiwemo za afya zimezidi kuzorota, huku vituo 10 vya afya Gedo sasa vimefungwa kutokana na mapigano.