Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waonya juu ya mienendo ya kulipiza kisasi kwa watetezi wa haki za binadamu

UM waonya juu ya mienendo ya kulipiza kisasi kwa watetezi wa haki za binadamu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ameungana na washirika wa kikanda kuzitaka nchi kukomesha mienendo yao inayokwamisha jitihada za watu binafsi na makundi mengine yanayotaka kushirikiana na Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kutetea haki za binadamu..

Mtetezi huru wa haki za binadamu Margaret Sekaggya amesema kuwa vitendo vya ulipizaji kisasi na visa vingine vinavyowaandama watu wanaotoa mchango wa kutetea haki za binadamu vimekwamisha kwa kiwango kikubwa ufikiaji shabaha ya kufichua vitendo hivyo.

 Amesema kasi ya mashirikiano baina ya taasisi za Umoja wa Mataifa na watetezi huru wa haki za binadamu, inapungua na hata baadhi ya maeneo majukumu ya kuchunguza uharibifu wa haki za binadamu yamedumaa kutokana na mbinyo huo kutoka kwa vyombo vya dola.

 Mtaalamu huyo ama amezitolea mwito serikali kuacha uhuru na upenyo kwa vyama vya kiraia ili vitoe mashirikiano ya karibu na Umoja wa Mataifa na washirika wake.