Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapongeza uamuzi wa ICC dhidi ya uhalifu wa kivita kwa watoto

UNICEF yapongeza uamuzi wa ICC dhidi ya uhalifu wa kivita kwa watoto

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limepongeza uamuzi wa leo wa mahakama ya ICC kumkuta na hatia Thomas Lubanga ya uhalifu wa kivita kwa kwaingiza watoto katika jeshi lake nchini DR Congo.

UNICEF inasema kuwa uamuzi wa leo Lubanga amekuwa mbabe wa kwanza wa kivita kukabiliana na mkono wa kimataifa wa sheria kwa kuwatumia watoto kama silaha ya vita.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake hatua ya leo ni ushindi mkubwa katika kuwalinda watoto kwenye maeneo ya vita, na utatuma ujumbe muhimu na wa wazi kwa makundi yenye silaha kwamba kuwafanya watoto watumwa na kuwatendea ukatili, ni jambo lisilovumilika.

Lake amesema watoto wengi wasiojiweza hutumbukia katika mikono ya watu kama Lubanga hasa watoto yatima au wale ambao wametenganishwa na wazazi wao, familia na jamii zao kutokana na vita.

Na UNICEF imekuwa ikitoa ombi kila wakati kuhakikisha wale wote wanaowatendea watoto ukatili na unyama wachukuliwe hatua kali ili iwe mfano kwa wengine.