Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu maswala ya uzazi kuandaliwa mjini London

Mkutano kuhusu maswala ya uzazi kuandaliwa mjini London

Serikali ya Uingereza, shirika la Bill na Melinda Gates, mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wengine wanatarajiwa kushiriki kwenye  warsha itakayoandaliwa mjini London mwezi Julai ambapo watajitolea  kufadhili mahitaji ya upangaji uzazi kwa wanawake kwenye nchi maskini duniani.

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa UNFPA Babatunde Osotimehin amesema kuwa uhuru wa kuchagua ni watoto wangapi mmoja atazaa ni haki ya kibinadamu.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha haya masuala kama vile usawa wa kijinsia na afya ya uzazi yanastahili kuangaziwa.