Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa shirika la UNESCO waboresha makavazi barani Afrika

Mradi wa shirika la UNESCO waboresha makavazi barani Afrika

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO  kwa ushirikiano na shule inayohusika na masula ya utamaduni nchini Benin wamewapa mafunzo watu 33 kutoka makavazi 30 kutoka nchi 17 jinsi ya kutunza makavazi yaliyo kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara.

Programu hiyo inayofadhiliwa na shirika kutoka Japan inahusu mafunzo ya darasani yaliyochukua muda wa juma moja mwezi Agosti mwaka 2011 na kufuatiwa na mafunzo mengine ya miezi 18 kupitia kwa mawasiliano ya mtandao.

Pia warsha mbili za kutoa mafunzo ziliandaliwa mwezi Septemba mwaka 2011 nchini Togo  na Septemba mwaka uliopita nchini Gabon.