Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM eneo la Sahara Magharibi kufanya ziara ya eneo hilo mwezi Mei

Mjumbe wa UM eneo la Sahara Magharibi kufanya ziara ya eneo hilo mwezi Mei

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahara Magharibi ametangaza kwamba atalitembelea eneo hilo hasa eneo lilalozozaniwa.

Mjumbe huyo wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Sahara Magharibi Christopher Ross ameyasema hayo baada ya mazungumzo ya siku tatu akiongeza kuwa mikutano mingine itaandaliwa barani Ulaya mwezi Juni.

Umoja wa mataifa umekuwa mshirika mkubwa katika kutafuta suluhu kwenye eneo la Sahara Magharibi tangu mwaka 1976 wakati kulipotokea mapigano kati ya Morocco na eneo la Frente Polisario kufuata kuondoka kwa utawala wa kikoloni wa Uhispania.