Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa ya kiarabu yanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji

Mataifa ya kiarabu yanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji

Mataifa ya kiarabu sasa yametumbukia kwenye mkwamo wa ukosefu wa maji kutokana na ongezeko la kasi la watu na kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya chakula.

Pia kumetajwa mambo mengine ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, matukio yanayokwenda sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa na kuharibiwa kwa mara kwa mara kwa miundo mbinu inayosambaza maji, kuwa ni baadhi ya mambo yaliyozusha sokomoko hilo.

Kutokana na hali hiyo, Umoja wa Mataifa unahimiza haja ya kuongeza mashirikiano ya haraka na kutaka pande zote kukaribisha mashirikiano ya matumizi ya maji yanayopatikana kwenye vyanzo vichache vilivyopo sasa.

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Umoja huo wa Mataifa inayoangazia hali ya upatikanaji wa maji, imesema kuwa hata hivyo mataifa ya kiarabu yameimarisha kazi ya kukabiliana na changamoto hiyo.