Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS, UNDP waipongeza New Zealand kutokana na mbuni zake za kukabili maambukizi ya HIV

UNAIDS, UNDP waipongeza New Zealand kutokana na mbuni zake za kukabili maambukizi ya HIV

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameipongeza New Zealand kutokana na ilivyochukua mkondo sahihi kushughulikia tatizo la mambukizi ya virusi vya HIV.

Wakurugenzi watendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS, na lile la maendeleo UNDP wamesema kuwa serikali ya New Zealand imechukua mkondo wa kuridhisha hasa kutokana na hatua yake ya kutoa kipaumbele kwa makundi ya watu walioko hatarini kupata maambukizi  wanapatiwa usaidizi wa haraka.

 Wakishiriki kwenye mkutano wa pamoja,  Michel Sidibé wa UNAIDS, Helen Clark kutoka UNDP walimwagia sifa waziri mkuu John Key na kusema kuwa serikali yake imechukua hatua madhubiti kukabili kusambaa kwa maambukizi ya virusi hivyo.

 Itakumbukwa kuwa New Zealand ni miongoni mwa nchi za kwanza kuanzisha huduma ya usaidizi kwa wale wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya.

Hatua hiyo imesaidia pakubwa kupunguza  maambukizi ya HIV.