Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wa usalama wa chakula kuonyesha hali mbaya ya njaa Yemen

Utafiti wa usalama wa chakula kuonyesha hali mbaya ya njaa Yemen

Upungufu wa chakula nchini Yemen umefikia kiwango cha hatari huku watu takribani milioni tano hawawezi kuzalisha au kununua chakula wanachokihitaji.

Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya awali ya utafiti uliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na kitengo cha taifa cha takwimu cha Yemen na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

 Mwakilishi wa WFP Yemen Lubna Alaman amesema njaa inaongezeka Yemen, huku ongezeko la bei ya chakula na vita vikiathiri watu wengi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)