Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICC yamkuta na hatia Thomas Lubanga wa DR Congo

Mahakama ya ICC yamkuta na hatia Thomas Lubanga wa DR Congo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imemkuta na hatia ya uhalifu wa vita bwana Thomas Lubanga.

Miongoni mwa makosa yaliyomtia hatiani Lubanga mbabe wa zamani wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kuwaingiza watoto jeshini ili kushiriki mauaji na mashambulizi kwenye jimbo la Itri Mashariki mwa nchi hiyo.

Majaji wanasema alipokuwa mkuu wa kundi la waasi la FPLC, Lubanga alihusika na kuwaingiza kwa hiyari au kwa nguvu jeshini wavulana na wasichana waliokuwa na umri wa chini ya miaka 15.

Majaji wameongeza kwa mara kadhaa Lubanga alikuwa akitoa hotuba zilizowachagiza watoto kujiunga na kundi lake la waasi ili kutoa usalama kwa raia. Jaji Adrian Fulforl ndiye aliyesoma uamuzi wa mahakama hii leo.

(SAUTI YA JAJI ADRIAN FULFORD)