Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yafadhili msaada kwa watoto wa Chad waliokwama kwenye mpaka na Nigeria

Marekani yafadhili msaada kwa watoto wa Chad waliokwama kwenye mpaka na Nigeria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM lina mipango ya kutuma msafara unaosafirisha misaada kwa zaidi ya wahamiaji 1000 wengine wakiwa ni watoto wasio na wazazi waliokwama kwenye kijiji cha N’Gbouboua eneo la Lac Magharibi mwa Chad.

Ubalozi wa Marekani nchini Chad umekubali kufadhili usafirishaji pamoja na shughuli ya kuziunganisha familia. Pesa hizo pia zitaliwezesha shirika la IOM kununua bidhaa muhimu kama mablankti, sabuni , matandiko ya kulalia pamoja na madawa kwa wahamiaji hao.

Wanafunzi wanaosoma kitabu cha Koran pamoja na walimu wao walivikimbia vijiji vilivyo mashariki mwa Nigeria vya Dougouri, Folkine, Koyoron na Malfahtri majuma matatu yaliyopita kufuatia mapigano kati ya kundi la Kiislamu la Boko Haram na vikosi vya Nigeria. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM na anafafanua zaidi.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)