Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuituma timu ya wachunguzi wa haki za binadamu kwenye mipaka ya Syria

UM kuituma timu ya wachunguzi wa haki za binadamu kwenye mipaka ya Syria

Umoja wa Mataifa utatuma timu ya waangalizi wa haki za binadamu katika nchi zinazopakana na Syria ili kukusanya taarifa za uhalifu na ukikwaji wa haki za binadamu unaotekelezwa nchini Syria. Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kyung-wha Kang amesema waangalizi hao watapelekwa baadaye wiki hii.

Ameongeza kuwa vyunzo vingi vinavyotoa taarifa kwenye ofisi ya haki za binadamu kuhusu kinachotolea Syria hasa katika ukiukaji wa haki za binadamu wanahofia vimetoweka. Bi Kanga ameyasema hayo katika hitimisho la mjadala wa baraza la haki za binadamu kuhusu ripoti ya tume ya uchunguzi dhidi ya Syria.

(SAUTI YA KUNG-WHA-KANG)

“Hadi kufikia Desemba tulikuwa na vyanzo kadhaa vilivyokuwa vikipasha habari ofisi yetu kutoka nchini humo, lakini baada ya Desemba vyanzo hivyo vikatoweka. Tunajaribu kudumisha mawasiliano na ndani ya nchi hiyo kadri tuuwezavyo. Tutapeleka ujumbe wa waangalizi ili kukusanya taarifa na kuorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo ya mipakana na nchi jirani baadaye wiki hii. Kuna uungwaji mkono mkubwa kuitoka kwa wajumbe wa baraza wa kuongeza muda wa tume ya uchunguzi na ofisi ya haki za binadamu iko tayari kuisaidia tume hiyo katika hatua nyingine ya shughuli zake.”