Annan asema anatarajia kupata jibu kutoka Syria hii leo

13 Machi 2012

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kiarabu nchini Syria Kofi Annan anasema kuwa anatarajia kupata majibu kutoka kwa serikali ya Syria kutoka na mapendekezo aliyowasilisha kwao. Akiongea mjini Ankara baada ya kukutana na waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan Annan amesema kuwa mara atakapopokea jibu lao ndipo atakapofanya uamuzi wake.

Hata hivyo Annan anasema kuwa ghasia na mauaji ni lazima vikomeshwe akiongeza kuwa wananchi wa Syria wamepitia mengi yaliyo magumu na sasa wanahitaji maisha mema. Amesema kuwa wajibu wake mkuu ni maslahi ya wananchi wa Syria na taifa la Syria.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter