Muafaka waafikiwa kuhusu umiliki wa ardhi na fursa za uvuvi na misitu:FAO

13 Machi 2012

Mazungumzo ya kimataifa yaliyofanyika kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo FAO wiki iliyopita ili kukamilisha majadiliano ya mapendekezo ya muongozo wa kimataifa kuhusu kudhibiti umiliki wa ardhi na fursa za haki ya kuwa na ardhi, uvuvi na rasilimali ya misitu yamemalizika kwa mafanikio.

Muuongozo uliopendekezwa sasa uko tayari kufikiriwa kwa idhini ya mwisho na kamati ya kimataifa ya usalama wa chakula CFS katika kikao maalumu kinachofanyika leo mjini Roma Italia.

Mwenyekiti wa CFS Yaya Olaniran amesema mara muongozo huo utakapoidhinishwa utakuwa ni wa hiyari lakini kwa kuwa umeaandaliwa kwa kushirikia wadau wote anaamini utatoa hamasa kubwa kwa watunga sera.

Muongozo huo unaelezea misingi na mwenendo ambao serikali na wadau wengine wanapaswa kuutumia wakati wakishughulikia masuala ya ardhi, uvuvi na haki za rasilimali za misitu ili kukidhi mahitaji na matakwa ya watu wake, kuchagiza usalama wa chakula na maendeleo vijijini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter