Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu ajadili umuhimu wa UM akiwa kwenye bunge la Ulaya

Rais wa Baraza Kuu ajadili umuhimu wa UM akiwa kwenye bunge la Ulaya

Akiwa katika bunge la Umoja wa Ulaya, rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ametaja vipaumbele vinavyozingatia na Umoja huo katika wakati ambapo hali jumla ya dunia ikiwa kwenye mkwamo wa mambo.

 Rais huyo amejadilia nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kuzishughulikia changamoto na mikwamo inayoendelea kuiandama dunia kwa wakati huu na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa umesalia kuwa matumaini ya wengi.

Amesema katika nyakati hizi ambazo zinashuhudiwa maingiliano ya mambo na kuzuka kwa changamoto mbalimbali, Umoja wa Mataifa unasalia kuwa chombo kinachounganisha matakwa ya dunia.

Kuhusu hali ya mambo iliyozikumba nchi za Kaskani mwa Afrika,  Bwana  Al-Nasser ameitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kuzipiga jeki nchi hizo za kiarabu hasa wakati huu zinapopitia kwenye kipindi cha mageuzi ya kidemokrasia.