Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa ECOSOC ataka nchi kuwa na maingiliano ya sera za uchumi

Rais wa ECOSOC ataka nchi kuwa na maingiliano ya sera za uchumi

Rais wa baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya uchumi na jamii ECOSOC amezitolea mwito nchi mbalimbali duniani kutekeleza kwa vitendo sera zitakazosaidia kustawisha kwa hali ya uchumi.

Miloš Koterec, amesema dunia inapaswa kuwa na shabaha moja ya kusukuma mbele uchumi wake na inaweza kufaulu kufanya vyema kama kutakuwa na utashi wa pamoja na kuowanisha sera zinazozingatia hali ya uchumi.

Amesema kuna haja ya kuwa na mafungamano ya pamoja kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya kiuchumi ambako pia kutafungua milango ya ajira.

Ametaka kubuniwa kwa mipango itakayoangazia kuzikabili changamoto katika kipindi cha muda mfupi, lakini pia kuweka mikakati itayomulika mambo kwa vipindi vya kati na virefu pia.