Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amtaka rais wa Syria kuchukua hatua kumaliza ghasia

Ban amtaka rais wa Syria kuchukua hatua kumaliza ghasia

Rais wa Syria Bashaar Al-Assad ametakiwa kuchukua hatua maramoja kukomesha ghasia, ukiukaji wa haki za binadamu na kushughulikia matatizo ya kibinadamu.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumatatu wakati wa kikao cha baraza la usalama kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Assad pia ametakiwa kuchukua hatua muafaka kufuatia mapendekezo ya amani yaliyowasilishwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiaraabu Kofi Annan.

Ban Ameonya kwamba machafuko yanayoendelea Syria yanaweza kuiweka kanda nzima katika hali ya hatihati.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia ameliomba baraza la usalama kushikamana na kuunga mkono mpango wa amani wa Kofi Annan. Amezipongeza Urusi na Uchina kwa juhudi zao za kujihusiha Syria na Umoja wan chi za Kiaarabu katika kutafuta suluhu ya machafuuko.