Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waendelea na jitihada za kuwalinda raia kutoka kwa kundi la LRA

UM waendelea na jitihada za kuwalinda raia kutoka kwa kundi la LRA

Katibu kwenye masuala ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema kwamba vikosi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikitoa huduma za kuwasindikiza wafanyibiashara kwenda sokoni pamoja na wale wanaohudhuria ibada kanisani.

 Akielezea jukumu la Umoja wa Mataifa katika shughuli za kukabilina na kundi la Lord’s Resistance Army LRA wakati wa mahojiano na kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Ladsous ameongeza kuwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikipiga doria vijijini na mijini na sehemu waliko LRA.

Kundi la LRA lilibuniwa miaka ya themanini nchini Uganda na kwa zaidi ya miaka 15 limekuwa likiwavamia raia wa Uganda na vikosi vya usalama.