Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wafungwa 600 wamenyongwa Iran mwaka 2011

Zaidi ya wafungwa 600 wamenyongwa Iran mwaka 2011

Zaidi ya wafungwa 600 wamenyongwa nchini Iran mwaka 2011 amesema mtaalamu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu.

Ahmed Shaheed ambaye ni mwakilishi maalumu wa haki za binadamu nchini Iran amesema wafungwa hao wamenyongwa bila kupewa fursa zinazostahili za kisheria ikiwemo uwakilishi wa mawakili.

Akihutubia baraza la haki za binadamuu mjini Geneva bwana Shaheed amesema uhuru wa vyombo vya habari unabanwa sana huku waandishi habari zaidi ya 42 wakishikiliwa kwa madai ya makosa ya kisalama.

Amesema ingawa Iran imekataa ombi lake la kuzuru nchi hiyo amekusanya ushahidi kwamba ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unafanyika ikiwemo watu kuwekwa kizuizini, kuteswa, kunyimwa uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

(SAUTI YA AHMED SHAHEED)