Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sehemu zinazopokea madawa ya Ukimwi zashuhudia viwango vya chini vya maambukizi

Sehemu zinazopokea madawa ya Ukimwi zashuhudia viwango vya chini vya maambukizi

Watafiti kutoka kwa kituo cha afya na idadi ya watu kimetoa matokeo  yanayoonyesha  kuwa watu kwenye maeneo yanayopata madawa yanayopunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi hawako kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi hayo.

Mkurugenzi wa shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la  Umoja wa Mataifa UNAIDS Paul De Lay anasema kuwa matokeo ya utafiti huo ni muhimu ambapo amezitaka nchi na jamii kuwa na madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi hasa kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.