Mabadiliko kwenye sheria za maandamano ni tisho kwa haki za binadamu

9 Machi 2012

Mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa Maina Kiai amekashifu baadhi ya mabadiliko yaliyopendekezwa kwenye sheria za maandamano mjini Geneva akiongeza kuwa huenda mabadiliko hayo yakakandamiza haki ya uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujieleza.

Sheria hizo zinaruhusu kutolewa faini ya takriban dola 110,000 kwa yeyote ambaye hajapewa ruhusa ya kuandamana au kwa yeyote ambaye aheshimu amri ya polisi.

Sheria hizo pia zinasema kwamba yeyote ambaye aliruhusiwa kuandamana na maandamano hayo yakazua vurugu hata bila ya yeye kuhusika huenda akanyimwa kibali cha kuandamana kwa muda wa miaka mitano.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud