Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaomba dola milioni 68.9 ili kukabiliana na hali kwenye eneo la Sahel

FAO yaomba dola milioni 68.9 ili kukabiliana na hali kwenye eneo la Sahel

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa nchi zilizo kwenye eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika zinahitaji usaidizi wa dharura ili kuzuia hali ya uhaba wa chakula iliyo katika eneo hilo kuwa mbaya na kuziokoa jamii zinazotegemea mifugo na kilimo.

FAO inatoa ombi la dola milioni 69.8 ili kutoa usaidizi kwa familia 790,000 zinazotegemea kilimo cha mimea na ufugaji zizazokabiliwa na uhaba wa chakula. Hali hiyo inakisiwa kusababishwa na masuala mengi yakiwemo ukame, kupungua kwa mazao ya nafaka, bei ya ju ya nafaka, mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini.