Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yatoa dola milioni 26.7 kwa huduma za IOM mwaka 2012

Japan yatoa dola milioni 26.7 kwa huduma za IOM mwaka 2012

Serikali ya Japan imetoa ahadi ya msaada wa dola milioni 26.7 wa kufadhili huduma za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM zikiwemo za wahamiaji, jamii zinazowapa hifadhi wahamiaji waliorejea nyumbani, watu wanaosafirishwa kiharamu pamoja na wakimbizi wa ndani.

 Miradi itakayofadhiliwa nchini Afghanistan, Ivory Coast, Djibouti, Ghana, Kenya, Rwanda, Somalia na Zimbabwe itasaidia mataifa kudhibiti uhamiaji  kutokana na majanga ya kiasili na yaliyosabbishwa na binadamu.

Nchini Afghanistan dola milioni 10 zitatumika katika kuwapokea kwa watu wanaorejea nyumbani kutoka nchini Iran, katika kuwatambua na kuwasaidia watu wanaosafirishwa kiharamu na kuwasaidia waafghanistan walio nje kurudi nyumbani.

Dola zingine milioni 16.7 zitatumika kwenye huduma za kibinadanmu za IOM  zikiwemo dola milioni 12.7 zitakazofadhili huduma za IOM kwenye pembe ya Afrika.