Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazuru mji wa Baidoa nchini Somalia

WHO yazuru mji wa Baidoa nchini Somalia

Shirika la afya duniani WHO limeutembelea mji wa Baidoa nchini Somalia ambapo ulitwaliwa na vikosi vya serikali ya Somalia hivi majuzi.

WHO inatoa usaidizi kwa hospitali moja inayosimamiwa na shirika moja lisilokuwa la kiserikali la Italia ambapo imeweka vifaa vya upasuaji kwenye hospitali hiyo na kutoa mafunzo kwa wauguzi kuhusu huduma za dharura.

Pia WHO inaeneza huduma zake kwenda maeneo ambayo yamekombolewa hivi majuzi ya kusini na kati kati mwa Somalia.