Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna usalama wa nishati ya nyuklia:UM

Kuna usalama wa nishati ya nyuklia:UM

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa taifa la Japan limepiga hatua kubwa.

Akiongea wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Japan katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa taifa la Japan limepiga hatua kubwa ya kuzoa na kutumia taka iliyotokana na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hyo mwaka mmoja uliopita. Ban amesema kuwa ameiunga mkono  Japan katika jitihada zake za ujenzi mpya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la nishati ya nyuklia la Umoja wa Mataifa Yukiya Amano anasema kuwa nishati ya nyuklia imekuwa salama  huku mataifa na serikali wakichukua tahadhari kubwa.