Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Syria ni ya kuhofisha:Amos

Hali nchini Syria ni ya kuhofisha:Amos

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valeria Amos amesema kuwa ameshtuka kutokana na aliyoyaona nchini Syria . Amos amesema kuwa karibu majengo yote yameharibiwa na hamna watu waliosalia akielezea wasi wasi wake kuhusu hatma ya watu waliolazimika kuhama mji wa Baba Amr.

Amesema kwamba alikutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Syria na mawaziri wengine serikalini ambapo alielezea hisia zake juu ya hali ilivyo nchini Syria. Ameongeza kuwa ni lazima kufanyike mikakati ya kuhakikisha kuwa mashirika ya kutoa misaada yanapewa fursa ya kuwahudumia waliojeruhiwa na kuwapelekea misaada waathiriwa.