Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo:UM

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo:UM

Haiti inapaswa kumteua Waziri Mkuu haraka iwezekanavyo ili kuepusha hali yoyote ya mkwamo inayoweza kujitokeza.

Akizungumza mbele ya baraza la usalama, mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini humo Mariano Fernandez amesema kuwa taifa hilo haliwezi kusonga mbele katika hali ya amani na utulivu kama nafasi ya waziri mkuu itaendelea kuwa wazi.

Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille alijiuzulu wiki mbili zilizopita ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kuchaguliwa kwake.

Kujiuzulu kwake kuliacha maswali mengi na kuzua hali ya shaka juu ya mustakabala wa taifa hilo.Wengi walitizama hali hiyo kama ni hali ya kukosekana kwa ukomavu wa kidemokrasia na hivyo kuzusha wasiwasi wa kuibua hali ya mkwamo wa mambo.