Kiu yangu ni kumkomboa mwanamke mwenzangu Burundi:Hafsa Mossi

9 Machi 2012

Wakati ulimwengu wiki hii umeadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake hapo Machi 08 ikiambatana na kauli mbiu kuwawezesha wanawake wa vijijini.

Burundi ni mojawapo wa mataifa ya Afrika ambayo yamepiga hatua kwa kuwapa kina mama nafasi kwenye ngazi mbalimbali ikiwemo mashirika, serikalini na taasisi  mbalimbali. Katiba ya nchi hiyo inasema kwa uchache uwakilishi wa akina mama katika uongozi wa ngazi zote uwe asilimia 30.

Kwa kiasi serikali imejitahidi kufikia lengo na mmoja wa wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa taifa nchini Burundi ni Bibi Hafsa Mossi.

Bi Hafsa mtangazaji wa zamani wa kimaitafa, ameweza kujinasua kwa kujikita katika siasa za nchi yake. Katika kipindi cha miaka sita, Waziri Hafsa Mossi amepitia nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Burundi ikiwa ni pamoja na kushikilia uongozi wa wizara kadhaa.

Bi  Hafsa Mossi kwa sasa ni waziri wa Burundi wa Afrika ya Mashariki. Baada ya mafanikio hayo, anasema kiu yake kubwa ni kumuinua mwanamke kwa kumuwezesha asiwe tegemezi akishirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa mbele katika harakati za kumuendeleza mwanamke wa Burundi.

Muandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA amezungumza na Bi Hafsa Mossi, kuhusu mafanikio, kazi zake na matarajio yake. Wasikilize

(MAHOJIANO NA HAFSA MOSSI)