Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yapokea msaada wa Helkopta toka Ukraine

MONUSCO yapokea msaada wa Helkopta toka Ukraine

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha operesheni yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, vimepokea helkopta moja toka kwa serikali ya Ukraine ambayo itasaidia kuimarisha shughuli zake kwenye eneo hilo.

Msemaji wa vikosi hivyo pamoja na kusifia hatua hiyo pia ameongeza kuwa kutolewa kwa msaada huo kutawezesha kuboresha shughuli za utoaji huduma kwa wananchi wa eneo hilo.

Vikosi hivyo MONUSCO vinakabiliwa na changamoto kubwa ya kuyafikia baadhi ya maeneo kutokana na mifumo ya kijiografia ya eneo hilo, lakini kutolewa kwa helkopta hiyo kunafungua mlango wa kusafiri umbali mkubwa zaidi katika shughuli zake za ulinzi wa amani.

Msaada huo wa Ukraine ni sehemu ya mwitikio wa mwito uliotolewa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon ambaye daima anayahimiza mataifa wanachama kupiga jeki vikosi hivyo ili vitekeleze vyema majukumu yake.