Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga ataka kuwe na usawa wa kijinsia na kuwajumuisha wanawake kwenye masuala muhimu

Mahiga ataka kuwe na usawa wa kijinsia na kuwajumuisha wanawake kwenye masuala muhimu

Siku ya kiamataifa ya wanawake ikiadhimishwa hii leo ofisi inayohusika na masuala ya kisiasa ya Umoja wa mataifa kuhusu Somalia UNPOS imeonyesha uzalendo wake kwa wanawake kote duniani hasa walio kwenye maeneo yanayokabiliwa na mizozo na kuunga mkono jitihada za wanawake za kuleta amani nchini Somalia, kwa wanawake walio ndani mwa Somalia na walio nje.

Kupitia taarifa yake kwa siku ya leo mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa  Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema kuwa lengo namba tatu kati ya malengo nane ya maendeleo ya milenia ni la usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake yakiwemo masuala ya elimu na kuwahakikishia haki sawa kwa wasichana.

Mahiga ameongeza kuwa ratiba ya mpango wa amani nchini Somalia umeguzia majukumu muhimu ambayo ni lazima yatekelezwe ili kumaliza kipindi cha mpito kitakachotoa fursa sawa kwa washikadau wote wakiwemo wanawake.