Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE kushiriki vilivyo kwenye kongamano la sita la maji

UNECE kushiriki vilivyo kwenye kongamano la sita la maji

Tume ya kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ulaya inatarajiwa kuchangia vilivyo kwenye majadiliano ya  kongamano la sita la kimataifa la maji ambalo linalotarajiwa kuandaliwa kati ya tarehe 12 – 17 mjini Maeseille nchini Ufaransa.

Kongamano hilo ambalo ni kubwa zaidi la maji duniani linaandaliwa baada ya miaka mitatu na zaidi ya washika dau 25,000 kutoka kote duniani wakiwemo mawaziri, wabunge, mashirika yasiyokuwa ya serikali na wengine wengi.

 Haki ya kuwa na maji na usafi ambayo ilitambuliwa na Umoja  wa Mataifa  na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 itakuwa ajenda kuu ya kujadiliwa kwenye kongamano hilo.