Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

UM waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na makundi mengine ya kiharakati pamoja na serikali ya Tanzania umeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima kulimanjaro kama ishara mojawapo ya kusuma mbele nafasi ya mwanamke huku ikipinga vitendo vya dhulma dhidi yao.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo, ambalo pia limewashirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali barani afrika waliopaza sauti zao juu ya kulinda haki za wanawake duniani kote.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika linaloshughulikia wanawake, Bwana John Hendra amepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali nyingi barani afrika ikiwemo Tanzania kwa ajili ya kusukuma mbele ustawi wa mwanamke.

Ametaja miradi ya kimaendeleo pamoja na sera zinazomulika ustawi wa mwanamke kuwa ni mfano mzuri ambao Tanzania inatekeleza sasa, ikiwemo ule unaohusu MKUKUTA na MKUZA ambayo yote kwa pamoja inazingatia usawa kwa mwanamke.

Akizungumzia umuhimu wa siku hii na tukio la kupanda mlima Kilimanjaro, Bi Salome Anyoti ambaye ni mratibu wa shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa amesema kuwa.

Kaandoni mwa hayo, wakati huu kunashuhudiwa maandamano yenye ujumbe unaochangiza wanawake wapewe nafasi kwenye mabaraza ya maamuzi. Kadhalika wachangiaji wengi kwenye makongamano yaliyofungamanishwa na siku hii wanatupia jicho mchakato ulioanzishwa sasa wa uandikaji wa katiba mpya, wakitaka wanawake wapewa fursa zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)