Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo kwa watoto ni ukiukaji wa haki zao:Pillay

Hukumu ya kifo kwa watoto ni ukiukaji wa haki zao:Pillay

Watoto wa umri wa chini ya miaka 18 kuhukumiwa kifo, kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa msamaha na adhabu nyingine kubwa ni ukikaji wa haki za mtoto amesema kamishina mkuu wa haki za binadamu .

Bi Navi Pillay amesema takribani nchi 90 duniani zimehalalisha adhabu ya viboko ikiwa ni pamoja na adhabu zingine kama kuwaponda mawe au kuwakata viungo kama njia za kuwaadhibisha watoto kwa uhalifu waliotenda.

Akizungumza katika mwanzo wa mjadala wa baraza la haki za binadamu kuhusu haki za mtoto siku ya Alhamisi Bi Pillay ameelezea masikitiko kwamba vyombo vya habari na mtazamo wa jamii kwamba uhalifu unaofanywa na watoto unaongezeka au unachagiza nchi kuchukua hatua za kuwawajibisha watoto hao wahalifu hatua ambazo zinaishia kukiuka haki za watoto.

 Mkuu huyo wa haki za binadamu amesema watoto wahalifu wasishilikiliwe kwa muda mrefu na lazima wapewe fursa za ushauri wa kisheria.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)