Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dini kubwa kitisho kwa dini ndogo: Bielefeldt

Dini kubwa kitisho kwa dini ndogo: Bielefeldt

Mtaalamu mmoja wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba dini kubwa zimetajwa kuwa kitisho cha kuangamia kwa dini zingine ndogo na katika kuwatenga waumini wa dini zingine.

Akiongea kwenye mkutano wa baraza la haki za binamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva ambapo aliwasilisha ripoti yake kuhusu uhuru wa dini na imani Heiner Bielefeldt amezitaka serikali kote duniani kuacha kutenga dini zingine.

Bwana Bielefeldt pia amesema kuwa kuheshimu uhuru wa dini au imani haiambatani na mipango ya uongozi kwa kuwa ni haki ya binadamu.