Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia yaomba kuingia Afrika Mashariki:

Somalia yaomba kuingia Afrika Mashariki:

Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.

Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia inasema kuwa wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na hali ya kiusalama nchini Somalia kuimarika na utulivu kuanza kushuhudiwa.

 Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan Kusini na Sudan Khartoum kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo azma ya Sudan kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imekataliwa.

Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha nchi tano: Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya kufanya biashara bila vikwazo vyovote kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu moja kufikia mwezi Juni mwaka huu wa 2012.