Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu aipongeza Ubelgiji

Rais wa Baraza Kuu aipongeza Ubelgiji

Rais wa baraza kuu ameipongeza Ubelgiji kutokana namna inavyokaribisha mafungamano ya kimataifa ikiwemo kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa kwa njia ya kushiriki kwenye utanzuaji wa mizozo na inavyomulika hali ya mambo huko Mashariki ya Kati.

Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa Ubelgiji ni mshirika muhimu wa Umoja wa Mataifa.

Ameeleza hayo kwenye risala yake aliyoitoa mbele ya Bunge la nchi hiyo.

Ameipongeza nchi hiyo ambayo ameilezea kuwa ni mfano wa kuigwa kwani imekubali kuwa makao makuu ya jumuiya nyingi za kimataifa  zenye maskani yake mjini Brussels.

 Amesema kwa hakika taifa hilo limejitambulisha katika upenu wa dunia namna lilivyotayari kuzikabili changamoto za wakati lakini kikubwa zaidi dhima yake inayotanuka sasa ya kushiriki kwenye michakato ya usakaji amani katika maeneo mbalimbali duniani.