Wanawake ni muhimu hasa wakati wa mizozo:Pillay

7 Machi 2012

Mary Kini, Angela Apa na Agnes Sil wanatoka kwenye familia tatu hasimu kwenye maeneo ya milima ya Papua New Guinea. Awali wanawake hawa walikuwa wamezuizwa na sheria za makabila yao za kufanya mazungumzo kati yao lakini walikiuka sheria hizo kisisiri na kuhatarisha maisha yao ambapo walikuta sokoni na kujadili mipango ya amani na kisha kuwavutia wengi ambapo walijitokeza na kueneza ujumbe wa amani.

Kwa sasa wanawake hao wamebuni shirika la kuubiri amani na kumaliza dhuluma dhidi ya wanawake ambalo hadi sasa limekuwa maarufu katika eneo hilo. Huku siku ya kimataifa ya wake ikiadhimishwa hiyo kesho takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa ni asilimia 19.3 ya wanawake waliokuwa bungeni mwaka uliopita kote duniani.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud