Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OIC yaliambia Baraza la Haki za Binadamu inapinga mjadala wa mapenzi ya jinsia moja

OIC yaliambia Baraza la Haki za Binadamu inapinga mjadala wa mapenzi ya jinsia moja

Na nchi wanachama wa shirika la shirikiano kwa nchi za Kiislam OIC wamesema wanataka kudhihirisha msiamamo wao wa kupinga mada inayojadiliwa katika kazi za baraza la haki za binadamu, mada ambayo ni kukomesha ghasia na ubaguzi dhidi ya wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Kwa niaba ya nchi wanachama wa OIC mwakilishi wa Pakistan kwenye baraza la haki za binadamu amesema upinzani wao unatokana na ukweli kwamba tata katika suala la mfumo wa hisia za kimapenzi halieleweki na ni la kupotosha. Amesema suala hilo halina maafikiano ya maana yake na wala misingi ya kisheria katika sheria za kimataifa. Amesema Jumuiya ya kimataifa inatambua tu haki ambazo zimeorodheshwa katika azimio la haki za binadamu ambazo zilipitishwa na chombo cha haki za binadamu.

(SAUTI YA MWAKILISHI WA PAKISTAN)